Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rick Ross akabidhiwa funguo za Jiji la Miami

Rick Ross Miami Rick Ross akabidhiwa funguo za Jiji la Miami

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meya wa jiji la Miami Francis Suarez na Mbunge Frederica Wilson kutoka nchini Marekani siku ya Jana, Januari 15 wamemkabidhi ‘Rapa’ Rick Ross ufunguo wa jiji la Miami, huku akitangazwa kuwa muziki wake utaingia katika maktaba ya Congress.

Ross siyo msanii pekee ambaye ametunukiwa ufunguo wa heshima katika mji aliotokea, ikumbukwe kuwa wapo ma-staa ambao pia wamewahi kutunukiwa heshima hiyo akiwemo ‘rapa’ Drake, Wiz Khalifa na mwengineo.

Maktaba ya Congress ndiyo maktaba kubwa zaidi duniani, ikiwa na mamilioni ya vitabu, filamu na video, nyimbo, picha, magazeti na ramani. Maktaba hiyo inatumika kama chombo kikuu cha utafiti cha Bunge la Marekani na makao ya Ofisi ya hakimiliki ya U.S.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live