Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rick Ross aIjibu diss-track ya Drake iliyovuja wimbo mpya

Mwes Asfg Rick Ross aIjibu diss-track ya Drake iliyovuja wimbo mpya

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika ulimwengu wa muziki wa rap, drama haziwezi kuepukwa. Baada ya drama za J. Cole na Kendrick Lamar, Rick Ross na Drake wamegeukiana, huku Rick Ross akitafsriwa kama alimsubiri Drake kwa hamu sana. Ni kupitia “Champagne Problems,” wimbo mpya ambao Rozay ameutumia kum-diss Drake.

Drake alijikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kutokea kwa wimbo wake uliovuja kusikika akiwaiss Rick Ross pamoja na wasanii wengine wakubwa kama Kendrick Lamar na Future. Ndani ya muda mfupi, Rick Ross alitengeneza jibu lake kupitia wimbo huu mpya ambao ulichapishwa na DJ Akademiks kwenye livestream yake.

Wimbo wa “Champagne Problems” unatumia sampo ya sauti ya Drake akisema kuwa Rick Ross ni mtu anayempenda kushirikiana naye katika muziki. Hata hivyo, Rick Ross anatumia fursa hii kutoa mashambulizi yake kwa Drake kwa njia ya maneno makali na ya moja kwa moja.

Katika wimbo huo, Rozzay anadai kwamba Drake alifanya upasuaji wa pua na alituma barua ya kusikitisha na kuiacha kwa French Montana, hali ambayo imesababisha Rick Ross kum-unfollow French Montana kwenye mitandao ya kijamii.

Mbali na hilo, wimbo huu wa Rick Ross pia unatoa maoni yake juu ya mtindo wa muziki wa Drake kwa kusema: “Flow ni copy & paste, Weezy alikupa juice / Kijana mwingine mzungu kwenye bustani anayetaka kushirikiana na kundi.” Hii ni sehemu ya majibu ya moja kwa moja ya Ross kwa kile anachokiita kuwa ni ushawishi mkubwa wa Lil Wayne kwa Drake.

Kufuatia mzozo huu, mashabiki wa muziki wa rap wanaendelea kujadili na kusubiri kuona jinsi Drake atakavyorejea katika bifu hili na jinsi uhasama huu utakavyobadilika katika siku zijazo.

Kwa ujumla, mzozo huu unaonyesha jinsi drama katika ulimwengu wa muziki wa rap inavyoendelea kuwa sehemu ya utamaduni wa muziki huo. Mashabiki wanabaki kusubiri maelezo zaidi na kuona jinsi bifu hili litakavyokwisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live