Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rich Mavoko azungumzia ujumbe wake wa kifo ulioshtua wengi mtandaoni

48165 Pic+mavoko

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msanii Rich Mavoko amefunguka kwa mara ya kwanza alichomaanisha katika ujumbe wake ulioshtua wengi hivi karibuni aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Rich ambaye jina lake halisi ni Richard Martin, amesema alichomaanisha katika ujumbe huo ni tofauti na watu walivyomwelewa, huku akieleza kwamba hawalaumu kwa kuwa limechangiwa na nchi kupatwa na misiba mfululizo.

Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Rich aliandika maneno mafupi yaliyoambatana na picha ikimuonyesha amejiinamia “Ni siku ya mwisho ya maisha yangu yaliobaki” maneno yaliyoibua gumzo huku wengine wakimtakia apumzike kwa amani kwa kuandika maneno mafupi ya Kingereza RIP.

Katika mahojiano na Mwananchi, msanii huyo ambaye anatesa na wimbo wa ‘Wezere’ amesema katika ujumbe huo alioundika Machi 16 siku ya Jumapili, alikuwa anamaanisha kuwa siku hiyo haitakaa ijirudie.

“Mfano leo ni siku ya Alhamisi, ni wazi kwamba hakuna Alhamisi nyingine kama hii itakayojirudia, ndicho nilichokuwa ninamaanisha wakati naandika ujumbe huo, na mbona ni vitu vinaimbwa kwenye nyimbo mbalimbali, vinaandikwa kwenye vitabu labda kwa kuwa wengi wetu sio wapenzi wa kusoma,” alisema.

“Lakini kwa wengine wanaojua kuchanganua mambo nina imani waliposoma neno kwa neno walinielewa nini nilimaanisha na hao wanaodhani labda nilikuwa nataka kufa, wapi niliaga kuwa nakufa?”

Alipoulizwa kama ujumbe huo hakuleta athari kwa ndugu na watu wake wa karibu, Rich alisema hakupata usumbufu wowote kwa kuwa wanaomjua hawakuwa na wasiwasi iwapo kuna jambo linalomsumbua.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwaeleza mashabiki wake kuwa yuko vizuri na kuwaomba waendelee kumuunga mkono katika kazi zake.

Habari zote na Nasra Abdallah



Chanzo: mwananchi.co.tz