Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rich Mavoko: Sijawahi kuomba kurudi WCB

Mavoko X Mondi Rich Mavoko: Sijawahi kuomba kurudi WCB

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa Bongofleva, Rich Mavoko amesema alishtushwa na taarifa zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa ameomba msamaha ili arudi kufanya kazi na WCB Wasafi.

Mavoko ambaye alitoka WCB mwaka 2018, alisema alisikia taarifa hizo za kizushi kupitia mdogo wake lakini baada ya kufuatilia aligundua ni uongo hivyo akapuuzia.

"Sijawahi kujaribu kuomba msamaha na hakuna kitu kama hicho, bora nivae shati lililochanika kuliko kutembea tumbo wazi, kikubwa naomba mashabiki zangu waendelee kunipa sapoti kupitia wimbo wangu mpya Usizuge.” amesema Mavoko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live