Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ricardo Momo afunguka sakata la Rayvanny kulipishwa milioni 50

MOMO Ricardo Momo afunguka sakata la Rayvanny kulipishwa milioni 50

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaka wa Diamond, Ricardo Momo amezungumzia sakata la msanii aliyekuwa lebo ya Wasafi, Rayvanny kwa kufafanua namna ambavyo mikataba ilivyo.

Akiizungumzia mikataba iliyopo Wasafi, Momo alisema inakuwa na vipengele viwili ambapo cha kwanza ni mkataba wa kusimamia kazi na mwingine ni wa haki miliki ya kazi zako.

“Unaweza ukavunja mkataba wa kusimamiwa kazi zako na ukawa huru kufanya shoo zako na mambo mengine lakini kama hujavunja, lazima ubanywe.

“Lakini ili uwe huru zaidi pia lazima uvunje kipengele cha haki miliki ya platform zako ambazo zinakuingia mapato kama vile YouTube na mitandao mingine inayoingiza fedha. Sasa ili uweze kutoka jumla lazima umalizane katika maeneo yote mawili,” anasema Momo.

Momo alisema yawezekana Rayvanny alivunja mkataba wa kazi na ndio maana alitangaza kuwa yupo huru lakini akawa amebakisha kile kipengele cha pili cha kumfanya amiliki haki miliki ya mitandao ya kuuzia muziki hivyo akilipa vyote atakuwa huru sasa kumiliki kila kitu.

Sakata hilo limekuja mara baada ya kuvuja kwa taarifa kutoka kwa mtangazaji Mwijaku ambaye alisema, Rayvanny amelipishwa shilingi milioni 50 na Wasafi baada ya kuonekana kwenye shoo ya Nandy Festival hivi karibuni.

Hata hivyo, Rayvanny hajaweka wazi kama ni kweli amelipishwa kiasi hicho cha pesa au la lakini zaidi ameeleza kuwa, yupo huru kufanya kazi na mtu yoyote. Momo alipoulizwa kama ni kweli Rayvanny amelipishwa shilingi milioni 800 ili kumalizana na Wasafi jumla, alisema hizo ni habari tu zisizo na uhakika hivyo watu wasubiri wahusika wa Wasafi watakapoliongelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live