Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ricardo Momo afunguka alivyompokea Harmonize WCB, akawavuruga

Ricardo Momo  Harmonize WCB Ricardo Momo afunguka alivyompokea Harmonize WCB

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaka wa CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Ricardo Momo ameamua kufunguka namna alivyompokea msanii Harmonize siku ya kwanza kabla hajapokelewa WCB, lakini mwisho wa siku alivyoondoka ikawa kama bifu.

“Ukitazamana wasanii wote Top 10 Tanzania utakuta wametoka WCB ambao ndio wamepita kwenye mikono ya Doiamond Platnumz. Kwa wasanii hao Diamond hakufanya biashara tu, aliwekeza akili, utu na upendo ndani yake.

“Kuna mwaka Diamond alikaa mwaka mzima na nusu bila kutoa wimbo wowote akifanya tu kolabo na wasanii wake ili na wao wakue wafikie angalau level alipo, ndicho kipindi ambachgo Diamond alipigwa gepu na akina Davido na Wizkid.

“Ukiona hicho kitu halafu anakuja mtu uliyemsaidia anaona kama hakina thaani, kama binadamu utasema hapana. Mimi akija msanii sasa hivi simtaki hata kumpokea, sababu nilishawahi kufanya hisani yakanitokea.

“Kuna msanii aliwahi kuja nikampokea mimi, alianza kwa kumcheki Diamond WahtsApp akasema anaimba, ilikuwa Desemba 25, 2014 kwenye shoo ya Diamond wakati wa Sikukuu ya Krismasi pale Dar Live.

“Aliambiwa anicheki, akanipigia nikampokea pale Mbagala nikaingia naye ukumbini, nikachukua CD yake, akapanda stejini, akanitumia mimi clip, nikamwambia Diamond tusimwache huyu mtu anajua kuimba. Nikamchukua nikaja naye mpaka kwa Diamond, lakini Diamond alikuwa hataki hata kumuona.

“Nikabembeleza kumbe alikuwa hana hata pa kulala, tukamtafutia pa kulala, tukamuweka ofisini, lakini siku aliyoondoka Wasafi ndio mwanzo wa bifu mimi nay eye. Kuna wakati wasanii wanavunja mioyo, anakuja akiwa na shida kumbe moyo ana roho mbaya.

“Wengine hawawezi kuvumilia ndio maana wanatoa maneno makali kama Rommy Jones. Kumbuka kuwa huwezi kufunga milango ya watu wengine kusaidiwa na Diamond. Mungu kapanga mtu gani asaidiwe na Diamond. Hata mimi nikamwambia Diamond usifunge milango, ndio maana Babu Tale amesema tutasaini wasanii wengine wawili, lengo ni kuendelea kuwainua wasanii wachanga,” amesema Ricardo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live