Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ricardo Momo afunguka Wasafi kuwanyonya wasanii

Momo(1) Ricardo Momo afunguka Wasafi kuwanyonya wasanii

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kukiwa na minong’ono kuwa bosi wa lebo ya WCB, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anawanyonya wasanii wake, kaka wa msanii huyo, Ricardo Momo ameibuka na kuzungumzia suala hilo kwa undani.

Momo alianza kwa kusema, yeye ndani ya WCB, ni mmoja kati ya watu waliohusika kuwapokea wasanii karibu wote ndani ya WCB hivyo anafahamu ukweli wa mambo ulivyo.

“Watu wanasema tu haya mambo kwa sababu hawajui. Unajua Diamond ni mtu ambaye humwambii kitu katika suala zima la kumtetea msanii. Ikumbukwe kwanza, alijitoa utu wake hadi kuamua kumpokea msanii na kumgharamia.

“Yeye ni msanii halafu anawachukua wasanii maana yake amejitoa kumtangaza huyo msanii hata kama kibanadamu unaweza kuona labda anaweza kuja kuwa mkubwa kuliko yeye,” anasema Momo.

Momo amesema, msanii anapokuja, Diamond anaingia naye mkataba wakati ambao msanii husika anakuwa hajulikani. Anaingia mkataba wa kugawana naye mapato kabla hata haijajulikana lini hasa ataanza kupata faida.

“Anaweza kuweka mathalani shilingi Milioni 50, lakini msanii akawa anaingiza labda shilingi milioni mbili kwa shoo na hiyohiyo mgawane. Unaona hapo sasa ni jinsi gani atakaa na msanii huyo kwa hasara kwa muda mrefu,” anasema Momo.

Aliongeza kuwa, kwa kiasi kikubwa Diamond amekuwa muumini mzuri wa kutetea maslahi ya wasanii wake lakini pia kusimamia mikataba wanayoiweka siku ya kwanza na msanii.

“Wanatakiwa wawe wanasoma na kuelewa vizuri mkataba kabla ya kusaini,” anasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live