Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rhino wa The Mafik ageukia uimbaji wa Injili

Rhino Sdfv Rhino wa The Mafik

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: HabariLeo

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Uelewa wa Sauti aliyewahi kutamba kwenye Bongo Fleva na kundi la The Mafik kwa jina la usanii 'Rhino' ametangaza kuzindua albamu yake ya kwanza ya nyimbo za Injili Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam Uwelewa wa Sauti amesema kuwa jina la albamu hiyo ni 'Bila Chanzo Halisi Hutoboi'.

"Wanaoishi kwa kutazama nyuma maisha yangu ya zamani nimeshatoka huko sina ninachokumbuka ninachojua Bila Chanzo Halisi Hutoboi naishi maisha ya amani zaidi ya zamani," amesema msanii huyo.

Uwelewa wa Sauti amesema kuwa kuwa ni kweli ameokoka na hawezi kufanya maigizo na kueleza kuwa kwa sasa anaishi maisha mengine na hakumbuki maisha ya nyuma aliyoishi bila wokovu.

Chanzo: HabariLeo