Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rema analipwa Tsh bilioni 2.5 kwa shoo moja

Rema Artist Live Pic Rema analipwa Tsh bilioni 2.5 kwa shoo moja

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa tovuti ya Vanguard hivi sasa Rema anafanya show moja kwa dola milioni moja, hii ni sawa na bilioni 2.5 za Kitanzania.

Tovuti hiyo imeweka wazi kwamba kabla ya mwezi wa tano mwaka huu Rema alikuwa anatoza dola laki mbili kwa show, ila baada ya kufanya Remix ya "Calm Down" na Selena Gomez thamani ya Rema imepanda.

Tovuti imetaja baadhi ya matukio kama kutumbuiza usiku wa tuzo za Ballon d'Or, Show yake ya hivi karibuni 02 Arena ambapo tiketi zote ziliuzwa siku moja kabla ya Show, ushindi wa MTV Europe Music Award kipengele cha Best Afrobeats, Ushindi wa Billboard Music Award kipengele cha Top Afrobeats kumefanya nguvu na mvuto wa Rema uongezeke ndani ya muda mfupi, hivyo dau lake limepanda.

Ikumbukwe kiasi cha dola milioni moja ndicho anatoza Wizkid na Burna Boy, hivyo kwa sasa Rema ni "level" moja na wanamuziki hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live