Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za santuri zauza zaidi kuliko za CD Marekani

Rekodi Za Santuri Zauza Zaidi Kuliko Za CD Marekani Rekodi za santuri zauza zaidi kuliko za CD Marekani

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Mauzo ya rekodi za santuri za muziki yamekuwa ya juu zaidi kuliko rekodi za CD nchini Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987, kulingana na repoti mpya.

Zaidi ya rekodi milioni 41 za santuri ziliuzwa katika mwaka 2022, kwa bei ya $1.2bn (£.99bn).

Ni CD milioni 33 zilizouzwa pekee, ambazo ziliuzwa kwa $483m.

Ulikuwa ni mwaka wa 16 mfulurizo wa ukuaji wa mauzo ya rekodi, ikiwa ni takriban 71% ya mapato ta sampuli.

Mapato ya muziki yaliyorekodiwa nchini marekani yaliongezeka kwa miaka saba mfulurizo na kufikia $15.9bn.

Kwa ujumla, mapato ya rekodi ya muziki katika mwaka2022 yaliongezeka kwa 6%, kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirikisho la la sekta ya Kurekodi ya Marekani (RIAA), mapato haya yakipatikana kwa kiasi kikubwa kutokana na kusikilizwa kwa muziki mtandaoni lakini pia kutokana na mauzo ya muziki halisi.

Chanzo: Bbc