Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rehema Msuya anayeigiza sauti ya Helena Hatun

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Helena Hatun

Nafasi hii imechezwa na Cemre Ebuzziya. Ni muigizaji wa kituruki ambaye alishawahi kutamba kwenye filamu ya Bulanti na ile ya Wedding Dance ambazo zilitoka 2015.

Rehema Msuya

Rehema ananakilisha sauti ya Helena, msichana ambaye amewahi kutoka na Shehazard, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Sultan.

Helena ni msichana mzuri kwa sura alikuwa akiishi kijijini, lakini alipata nafasi ya kuingia katika kasri.

Walikuwa na mapenzi ya kweli, kwani alimpenda hata kabla ya kujua kwamba Shahazad ni nani. Japokuwa ndugu na wazazi hawakumkubali.

Mbali ya kunakilisha sauti, Rehema pia ni muandaaji na mtangazaji wa TV.

Malengo yake ya baadaye anasema ni kuja kuwa mtangazaji mkubwa wa kimataifa.

Ushauri wake kwa wasichana, amewasihi kutokubali kukata tamaa, kuwa wacha Mungu na kupambana kufikia malengo yao.

Kitu kingine anachokipenda mbali na utangazaji na kunakilisha sauti, anasema kwamba siku akifanikiwa atatimiza malengo yake ambayo ni kuwa na Shirika litakaloweza kuwasaidia kina mama na watoto na watu wenye mahitaji maalum.



Chanzo: mwananchi.co.tz