Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny kuja na Remix ya Chuchumaa

RAYVANNY FIESTA Rayvanny kuja na Remix ya Chuchumaa

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa kutoka Mbeya City, Raymond Mwakyusa 'Rayvanny' amesema anafikiria kuja na Remix ya wimbo wake maarufu wa Chuchumaa na kuomba mashabiki wamuambie nani anafaa kushirikiana naye.

Rayvanny ambaye kwa sasa amechomoka WCB na kufanya kazi kupitia lebo yake ya Next Level, ameandika mchongo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"MZIKI KITU CHA AJABU SANA YANI NIMEAMKA NAKUTA WIMBO WANGU WA #CHUCHUMAA UNA TREND SEHEMU TOFAUTI TOFAUTI DUNIANI IMAGINE WIMBO UNA MIAKA 3 ???????????? …..

LAZIMA NIFANYE VERSION MPYA YA HUU WIMBO JE NIIMBE NA NANI ????"aliandika Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live