Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny awaomba wanawake kumtongoza "Nipo singo"

RAYVANNY FIESTA Rayvanny

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Rayvanny amefichua kwamba yuko singo na tayari kusaka mchumba.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Rayvanny ambaye ni nyota wa nyimbo za Bongo amewataka wanawake wanaommezea mate kumtumia ujumbe wa moja kwa moja.

"Jamani kama unajijua ni binti mzuri na unanifaa, tafadhali naomba unitongoze," Rayvanny aliandika.

Msanii huyo wa kibao cha Zezeta alipigwa na bumbuazi baada ya simu yake kufurika jumbe za mahaba kutoka kwa wanawake waliokiri wanampenda.

Rayvanny alisambaza zaidi ya jumbe 50 alizopokea kwenye Insta Stories, na kufichua kuwa alikuwa amepokea zaidi ya jumbe 200 za mahaba kutoka kwa wanawake tofauti kwa saa chache tu. "Sikujua kwamba mnanipenda kiasi hiki.

Hata mimi nawapenda sana nyote. Leo nimekuja kugundua kwamba kweli dunia imejaa wanawake warembo sana. Ila mwisho wa siku siwezi kuw anao wote, nahitaji mwanamke mmoja tu.

"Nimepokea zaidi ya jumbe 200 za mahaba kutoka kwa wanawake tofauti kwa saaa chache tu, na zingine zinamiminika. Sikutarajia hili hata kidogo. Nawapenda sana nyote na ikiwa unanipenda pia nitongozee," msanii huyo wa Tanzania aliandika."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live