Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny atua nyumbani kwa Harmonize usiku kuchukua Tuzo yake

Rayvanny Mdas Rayvanny atua nyumbani kwa Harmonize usiku kuchukua Tuzo yake

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na C.E.O wa Nextlevel music Rayvanny amefika nyumbani kwa Harmonize usiku huu kuifata tuzo yake aliyoshinda Marekani kwenye Tuzo za AEAUSA, pia alipata nafasi yakufanya Maojiano (Interview) na waandishi wa habari nakufunguka mambo kibao.

Hii ni tuzo aliyoshinda Rayvanny katika kipengele cha best Collaboration kupitia video yake ya Mama Tetema aliyoimba na Maluma.

"Sio kwamba nilishindwa kwenda Airport kuchukua tuzo yangu au nilishindwa kuja hapa kesho nyie waandishi mkiwa hampo, nimekuja leo Konde Village kwa sababu ya ku-show love na kuonesha kwamba sisi ni ndugu na marafiki wala hatuna ugomvi.

"Nimewahi kugombana sana na Harmo tangu tukiwa kwenye Lebo lakini inafika wakati tunakuwa watu wazima, tunaamua kuua uaduai wetu na kushirikiana. Tunapaswa kugombana na dunia kwa ajili ya kuupaisha muziki wetu na sio kugombana sisi kwa sisi.

"Akina Rema ni watoto wadogo miaka 23 lakini wanakomba matuzo, sisi tunakalia ugomvi, haijengi. Nashukuru tuzo yangu nimeipokea salama salimini, asante sana Harmonize," amesema Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live