Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny atoa ya moyoni: Nimeheshimishwa

Rayvanny Mm rayvanny

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Masanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye pia ni CEO wa Next Level Music ameonyesha kuheshimishwa na kujawa na furaha baada ya kupata fursa ya kufanya shoo katika mkutano mkuu wa CAF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Mkutano huo ulijumuisha marais wa mashirikisho mbalimbali ya soka akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, Patrice Motsepe, waliombatana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Michezo, Mohammed Mchengerwa na wengine wengi.

Rayvanny amemshukuru pia Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo lakini aliwakilishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Vannyboy ameandika kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram kama ifuatavyo; “I am honoured to be part of CAF 44th ordinary General Assembly in My country ???????? ????❤️???????? #Globalway @caf_online @tffboard @wizara_sanaatz @gianniinfantino_ @fifaworldcup @tanzaniafootballfederation @tanfootball.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live