Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny atambulishwa rasmi Fiesta, atoa kauli nzito

RAYVANNY FIESTA Rayvanny

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye msanii maarufu wa Bongo Fleva, Rayvanny ametambulishwa rasmi kwenye Tamasha la Fiesta 2022 kuwa miongoni mwa wasanii watakaoangusha burudani la aina yake ikiwa ni miaka sita imetimia tangu msanii huyo apande kwenye jukwaa hilo kwa mara ya mwisho.

Hii inakuja ikiwa ni miezi michache tu baada ya Vanny Boy kujiondoa katika lebo yake ya zamani, WCB na kuamua kujitegemea kama msanii huru kupitia lebo yake mpya ya Next Level Music.

Ikumbukwe kuwa, akiwa WCB haikuwa rahisi kwenda kufanya shoo nje ya lebo hiyo bila utaratibu wa lebo husika kufuatwa, lakini kwa sasa sababu yuko huru imekuwa rahisi kwake kukubali kupafomu Fiesta.

Akizungumzia hilo, Vanny amesema; “Nimefurahi kuwa mmoja wa wasanii watakaopafomu Fiesta 2022, mara yangu ya mwisho ilikuwa mwaka 2016 kupanda kwenye jukwaa la Fiesta. Matamasha yanafanya wasanii kukutana hata kama mmemaliza siku nyingi, ku-show love na kuungana kwa pamoja.

“Kuwepo kwangu Fiesta hakuna tafsiri mbaya na uongozi wangu wa zamani (WCB) kwa sababu kila kitu kipo sawa.,” amesea Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live