Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny atakiwa kulipa milioni 50 WCB kisa kufanya shoo Nandy Festival

Rayvanny Tequ Rayvanny atakiwa kulipa milioni 50 WCB kisa kufanya shoo Nandy Festival

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Za ndani kabisa tulizozinyaka zinadai kuwa, CEO wa Next Level Music, Rayvanny anatakiwa kulipa pesa kiasi cha Tsh million 50 kwa iliyokuwa lebo yake, WCB Wasafi.

Malipo hayo ni kutokana na msanii huyo kupanda katika Jukwaa la #NandyFestival2022 la Msanii Nandy lililofanyika mjini Songea, hivi karibuni.

Inaelezwa kuwa, hii inatokana na Rayvanny kufanya show hiyo ikiwa bado hajafikia makubaliano ya kumalizana kikamilifu na label ambayo ilikuwa ikimsimamia ya WCB Wasafi.

Ikumbukwe kuwa, Rrayvanny aliondoka hivi karibuni WCB baada ya kufanya nayo kazi kwa miaka sita. Lakini baadaye taarifa zikasambaa kuwa tayari ameshamalizana na WCB baada ya kulipa kiasi cha Tsh milioni 800 alizotakiwa kulipa ili kuondpoka katika lebo hiyo.

Siku chache baadaye, Rayvanny na mabosi wake wa zamani, Diamond Platnumz na Sallam SK wote watatu kwa pamoja walionekana katika viunga vya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) huku kukitajwa kuwepo na kikao kizito cha makubaliano baina yao ili Rayvanny aweze kumalizana kikamilifu na WCB.

Kitendo cha kuonekana BASATA kilidhihirisha kuwa msanii huyo na lebo yake bado hawajamalizana kikamilifu licha ya pande zote mbili kutokuwa tamko lolote mpaka sasa iwapo wamemalizana au lah!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live