Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny anogewa kwa Fahyma

Rayvanny Na Fahyma Sd Rayvanny anogewa kwa Fahyma

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumtumia mama wa mtoto wake, Fahyma kama 'Video Vixen' na kupendezesha video ya wimbo wake wa #Forever, supastaa wa Bongo Fleva, Rayvanny amenogewa na mafanikio aliyoyapata kwenye video hiyo na ameahidi kumtumia Fahyma kwenye video ya wimbo wake mwingine kwa sababu ya uzuri wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye Instastory, Rayvanny ameandika; "Kwa jinsi alivyo mzuri nashoot nae my next video tena Forever haitoshi."

Ikumbukwe video ya wimbo wa Forever ilipata watazamaji 'Views" Milioni 1 ndani ya siku moja jambo ambalo linatajwa kuwa Fahyma ndio sababu kubwa kutokana na uwepo wake kwenye video hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live