Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny anatembelea nyota za wenzake kibiashara

RAYVANNY CRDB Rayvanny anatembelea nyota za wenzake kibiashara

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hivi karibuni Rayvanny amewekwa kitimoto na idadi kubwa ya mashabiki mtandaoni wanaodai amekuwa mwepesi wa kudandia nyimbo za wasanii wenzake zinazofanya vizuri kuliko kuwekeza ubunifu katika kazi zake.  

Kelele hizo zilizidi baada ya kuachia remix ya wimbo wa Dayoo 'Huu Mwaka' ambao unafanya vizuri sasa, wengi wanaamini Rayvanny anatembelea nyota za wasanii wenzake maana kila wimbo au tukio linaloibuka na kubamba basi atapita nalo.

Anachofanya staa huyo wa Next Level Music (NLM) ni kwamba anaposikia wimbo wa msanii fulani unafanya vizuri basi atamuomba afanye remix na ikibidi washirikiane, hadi sasa mbinu hiyo imempa Rayvanny kolabo zaidi ya 10 za ndani na nje.

Mpango huo upo kibiashara zaidi maana ndiye anagharamikia kila kitu ila kazi husika lazima iwepo kwenye majukwaa yake ya kidigitali hasa YouTube, na hapo ndio wakosoaji wake wanaona Rayvanny hana mpango wa kusaidia kama anavyodai. Ebu tazama;.

1. Rosa Ree & Rayvanny - Sukuma Ndinga Remix   Rapa Rosa Reee alipoachia wimbo wake, Sukuma Ndinga (2020) na kuanza kufanya vizuri, mara moja Rayvanny alimuomba remix, Rosa alikubali na hadi sasa video ya wimbo huo ambayo ipo YouTube kwenye chaneli ya Rayvanny ina 'views' 1.8 milioni.

Hata hivyo, Rosa Ree ambaye ni mshindi wa tuzo tano katika vipengele vya Hip Hop alisema hatua hiyo ni makubaliano ya menejimenti yake na ile ya Rayvanny na kuwa kazi hiyo inazinufaisha pande zote mbili.

2. Guchi & Rayvanny - Jennifer Remix Staa wa Nigeria, Guchi tayari alikuwa imeishika Afrika na wimbo wake, Jennifer (2021), Rayvanny alipousikia akavutiwa nao, basi akamgharamikia kila kitu Guchi akaja nchini na kurekodi remix yake pamoja na kushuti video.

Video yake tayari ina 'views' 21.7 milioni ikiwa ni video ya 12 kwa Rayvanny kutazamwa zaidi YouTube kwa muda wote, huku ikiwa kolabo yake ya pili ya kimataifa iliyofanya vizuri baada ya 'Teamo' (2020) akimshirikisha Messias Maricoa kutokea Msumbiji.

3. Mavokali & Rayvanny - Mapopo Remix Muda mfupi baada ya Mavokali kuachia wimbo wake, Mapopo (2022) ulifanya vizuri sana kimataifa na hata kuzizidi nyimbo nyingi za wasanii wakubwa Bongo, na punde tu Rayvanny akafanya remix yake.

Kama ni upepo au kutembelea nyota basi hapa Rayvanny alifanikiwa kwa asilimia 100, ila Mavokali akawa majanja kwa kuweka remix ya wimbo huo katika chaneli yake ya YouTube tofauti na wasanii wenzake na tayari ina 'views' 11. 2 milioni.

4. Lil Jay Bingerack & Rayvanny - Hi Hi Hi Remix Tunaelekea hadi Afrika Magharibi na kukutana na Lil Jay Bingerack kutokea Ivory Coast ambaye mwaka uliopita aliachia wimbo wake, Hi Hi Hi (2023) na kufanya vizuri baadhi ya maeneo Afrika.

Basi Rayvanny akaona hiyo ni nafasi ya yeye kupenya nchini Ivory Coast na Afrika Magharibi kwa ujumla, basi yeye na Lil Jay Bingerack wakatoa remix ya wimbo huo ambao video yake hadi sasa ina 'views' 1.2 YouTube katika chaneli Vanny Boy.

5. Chino Kidd & Rayvanny - Kibela Remix Kati ya wasanii Bongo ambao nyota zao ziling'aa mwaka uliopita, basi ni Chino Kidd, kila ngoma aliyotoa ilipata mapokezi mazuri, hakuna ubishi wimbo wake, Kibela (2023) akiwashirikisha S2kizzy na Mfana Kah Gogo ulipendwa na wengi.

Na kama kawaida Rayvanny akaona hiyo ni fursa wake, hakuna kingine zaidi ya kufanya remix ya wimbo huo na kuwapa shavu wote waliokuwepo mwanzo, huku video akiiweka katika chaneli yake na hadi sasa ina 'views' 2.3 milioni huko YouTube.

Pia ana mtindo huu Vilevile Rayvanny akiona tukio fulani linavuma katika tasnia basi atahakikisha analiweka katika muziki wake, mfano hivi karibuni alipoibuka DJ Misso Misondo na Wazee wa Makoti, mara moja akarekodi nao wimbo 'Kitu Kizito' na video kabisa wakatoa.  

Na kipindi Dudu Baya anavuma mitandaoni na harakati zake, Rayvanny mara moja akafanya naye wimbo, Konki (2018) na video ikaiweka kwenye chaneli yake YouTube na hadi sasa ina 'views' 1.1 milioni.   Jay Melody alipoibuka na wimbo wake, Huba Hulu (2021), Rayvanny akamuomba wafanye remix yake na tayari alishaanza kurekodi studio za NLM lakini ni kama Jay Melody alikuja kukataa mpango huo kwa kuona utamtoa kwenye mchezo wakati ndio ameanza.

Utakumbuka Jay Melody hana utamaduni wa kushirikisha wasanii katika nyimbo zake, ni jeshi la mtu mmoja na ngoma zake zinaenda mbali bila kolabo, wasanii wengi wanamuhitaji kuliko yeye anavyowahitaji kwa sasa.

Chanzo: Mwanaspoti