Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny amvalisha pete mrembo huyu

Rayvanny Mkl Rayvanny na mrembo huyo

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Bongo, Rayvanny amemzawadia shabiki wake pete wakati wa tamasha ambalo alifanya jijini Nakuru nchini Kenya wikendi iliyopita.

Shabiki huyo mwanadada alipanda jukwaani ambapo Rayvanny alikuwa akiwatumbuiza mashabiki na kumkumbatia mwanamuziki huyo.

Aliungana na staa huyo wa Bongo kuimba wimbo ambao alikuwa akicheza wakati huo huku akimuonyesha upendo. Rayvanny alifurahishwa na jambo hilo hadi kutoa pete aliyokuwa nayo na kumvalisha mwanadada huyo.

"Umeipenda," alimuuliza shabiki huyo baada ya kumvisha pete hiyo.

Baada ya tukio hilo, Rayvanny na shabiki huyo walipigwa picha pamoja huku mashabiki wengine wakishangilia jambo la kusisimua alilofanya mwimbaji huyo.

Hivi karibuni  mwimbaji huyo, kupitia Instastori zake alidokeza kuwa angependa kupendwa au kujitosa kwenye mahusiano.

Chapisho hilo lilipata hisia nyingi kutoka kwa baadhi ya wafuasi na mashabiki wake hasa wanawake ambao walionekana wakimiminika kwenye kikasha chake wakijaribu kurusha mistari kwa mahiri na mtunzi wa nyimbo huyo.

"Jamani kama unajijua ni binti mzuri na unanifaa, tafadhali naomba, nitongoze," Rayvanny aliandika.

Rayvanny amewahi kuwa katika uhusiano hapo awali. Walakini, kinyume na wengi, alichagua kwamba njia bora zaidi ya kufanya hivyo ni kuruhusu wanawake waje kwake na kujaribu kumtongoza.

Hata hivyo haijafahamika kama ilikuwa kweli msanii huyo alikuwa na hamu ya kujitosa kwenye mahaba au alikuwa anatafuta watazamaji wengi wa wimbo wake mpya wa Nitongoze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live