Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny amtaka Marioo kusema ukweli kuhusu kumuomba Diamond kumsaini WCB

Mariooooo Rayvanny .jpeg Rayvanny amtaka Marioo kusema ukweli kuhusu kumuomba Diamond kumsaini WCB

Sun, 29 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa @marioo_tz utakumbukwa kwa kuwa na burudani nyingi za matukio ya kila aina.

Msanii @rayvanny ni mmoja kati ya wasanii ambao walipanda kwenye jukwaa hilo na kufanya show ya nguvu lakini moja tukio ambalo lilipigiwa kelele ni la msanii huyo kumtaka Marioo kutamka kama hakumuomba Diamond Platnumz kumsaini kwenye lebo yake ya WCB.

Kauli hiyo iliufanya ukumbi huo ambao ulijaa maelfu ya watu kuzizima kwa shangwe. Hata hivyo Marioo ambaye alikuwa na furaha kubwa hakusema neno lolote.

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Diamond alisema kuwa, Marioo alimfuata na kumuomba Diamond amsaini kwenye lebo yake lakini baadaye ilishindikana. Jambo hilo liliibua mijadala huku Marioo akilikanusha na kusema hajawahi kuomba kusainiwa WCB.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live