Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny amfunika vibaya Harmonize

Rayvanny Na Harmonize Rayvanny amfunika Harmonize

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa unadhani Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amemfunika kwa kila kitu Rais wa Next Level na Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ unakosea, kuna kipengele cha YouTube, Rayvanny yupo juu zaidi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Socialblade ambao unaziweka kwenye mizani Youtube channel zote, Rayvanny anashika nafasi ya nne huku Harmonize akishika nafasi ya sita.

Habari ikufikie, namba moja inashikiliwa na Diamond Platnumz, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Wasafi Media nay a tatu ikishikwa na Millard Ayo huku namba nne ikienda kwa Global TV Online.

Rayvanny ana subscribes Milioni 3.91 huku Harmonize akiwa na subscribers Milioni 3.39M hivyo utaona ni jinsi gani Rayvanny ni mkubwa katika kipengele cha YouTube.

Kwa upande wa views, Rayvanny kwa mwezi amejikusanyia Milioni 17.011 huku Harmonize akiwa na views Milioni 12.146.

Wawili hawa wote walikuwa memba wa WCB kwa sasa wote wametoka, mpambano ndio umeanza nje ya lebo hiyo kubwa Bongo na sasa kila mtu anakuza ufalme wake, acha muvi iende tutaona nani zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live