Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny ameiheshimisha WCB ndani na nje ya nchi, hakustahili kukomolewa

Diamond Vanny B.jpeg Rayvanny ameiheshimisha WCB ndani na nje ya nchi, hakustahili kukomolewa

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lebo ya WCB Wasafi imejikuta katika vita kali mitandaoni baada ya madai kuibuka kwamba ilimtoza aliyekuwa msanii wake, Rayvanny kiasi kikubwa cha faini kwa kile ilisemekana ni msanii huyo kuhudhuria tamasha la Nandy lililofanyika Songea wiki mbili zilizopita.

Mtangazaji wa Clouds Media, Mwijaku alifichua kwamba hata baada ya Rayvanny kuweka wazi kuwa ameondoka Wasafi, ila bado hakuwa amekamilisha vipengele vyote vya kuondoka ili kuwa huru kabisa na moja ya sharti alilolikiuka ni kipengee kilichokuwa kikimtaka kutotumbuiza katika tamasha la msanii yeyote mshindani wa lebo hiyo kabla ya kuondoka rasmi, jambo ambalo anasemekana kulikiuka kwa kutumbuiza Nandy Festival.

“Mwanzo alipoambiwa alipe Tsh milioni 800 ili aondoke, alikubali kulipa. Lakini kukawa na mvutano kuhusu akaunti zake za mitandao ya kidijitali. Wakawa hawajamalizana bado. Yeye alisimamisha malipo ya Tsh milioni 800 ili wakubaliane kwanza kwa kuwa akilipa pesa zile zote watampa akaunti zake zote za kidijitali. Wale wana utaratibu, ukienda kwenye disco/klabu ama msiba, faini yake ni Tsh milioni 5, ukienda kwenye tamasha la wazi Tsh milioni 50," alisema Mwijaku.

Wiki jana Rayvanny alisemekana kuonekana katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na sasa inadaiwa kwamba alikwenda kule ili kupata usaidizi kutokana na faini hiyo kubwa aliyopigwa.

Wasanii mbalimbali sasa wamejitoa wazi na kumponda CEO wa WCB, Diamond Platnumz pamoja na lebo yake kwa kile wanachodai kuwa ni unyanyasaji mwingine zaidi ya ule wa lebo kuchukua 60% ya mapato ya kazi za wasanii.

“Rayvanny amewaheshimisha WCB Wasafi nchini na duniani kote. Ameshiriki tuzo za MTV, amefanya collabo za kimataifa, ameshinda tuzo ya BET miongoni mwa heshima nyingine nyingi za mafanikio.

“Kwa heshima hii, alikuwa anawadai kuondoka huru bila kulipia chochote na si kumchezea mchezo mchafu na kumkandia kama ambavyo wanamfanyia. Alilipa madeni yake! Lebo inafaa kuwa mtetezi wa wasanii na si mkandamizaji wa kukatisha tamaa za wasanii,” mwanamuziki Wakazi alilalama.

Msanii huyo wa Rap aliendelea kukemea kitendo cha Wasafi ambapo alisema kwamba hata lebo ya kimataifa kwenye miji ya watu kule Marekani Shady, Aftermath na Interscope zilikuwa kwa kipindi kimoja na msanii 50 Cent ila alipotoa albamu ya Grodt ambayo ilifanya vizuri zaidi ya maelezo, ilibidi lebo ile irudi kwenye mkataba na kuutathmini vizuri ili kumlipa 50 Cent alichokuwa anastahili kwa kuwa aliwaheshimisha kote ulimwenguni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live