Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny alipa mil. 20 hotelini

Rayvanny 2 Rayvanny

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAYMOND Shaban Mwakyusa au Rayvanny; ni staa mwingine wa Bongo Fleva anayefanya vizuri nje ya mipaka ya Tanzania ambaye kwa takriban siku kumi yupo jijini Paris nchini Ufaransa kwa shughuli za kimuziki.

Mbali na kufanya shoo baab’kubwa nchini humo, pia Rayvanny au Vanny Boy amekuwa studio na wasanii mbalimbali kama Adenkule Gold wa Nigeria ikiwa ni muendelezo wa kolabo zake za kimataifa.

Akiwa huko, Rayvanny ametoboa siri kwamba, anakaa kwenye hoteli ambayo analazimika kulipia shilingi milioni 2 za Kitanzania kwa siku hivyo kwa siku kumi alizokaa nchini humo zimemtoka shilingi milioni 20.

Rayvanny ameandika; “Imagine nipo hapa (hotelini) toka tarehe 7 (Machi), 2 milioni kwa siku chumba…”

Hata hivyo, hiyo inaweza isiwe habari kubwa kwani Diamond Platnumz; ambaye ni bosi wake kunako Lebo ya WCB anasema Rayvanny ndiye msanii wa pili kwenye lebo hiyo anayeingiza pesa nyingi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live