Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny ajisifu kuitendea haki video yake

RAYVANNY CRDB Rayvanny ajisifu kuitendea haki video yake

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii kutoka lebo ya Next Level, Rayvanny ameachia video ya wimbo wake mpya wa Vacation wikendi iliyopita.

Msanii huyo amejitapa kuwa video ya wimbo huo aliifanyia haki kwani alizunguka katika mataifa tisa ndani ya nje ya Afrika kwa ajili ya kufanya video hiyo.

Wimbo huo wenye maudhui ya ziara za kujivinjari ambao umetoka Jumapili alisema hakutumia kamera za kawaida bali katika mizunguko hiyo yote alitumia kamera ya simu kufanikisha maushui yake.

“Video ya Vacation imeshootiwa nchi tisa na simu tu,” Rayvanny alijitapa.

Rayvanny alisema alitembea kutoka nchi ya Tanzania, akaenda Marekani, akarudi ingereza, Uturuki na mataifa mengine kote duniani.

“Imagine video hii ilipigwa katika nchi 9 tofauti nzuri duniani kote ili kupata kitu kizuri kwa mashabiki wangu. Tulianza na Tanzania Mbeya, Morogoro na Mwanza, tukaenda Marekani Houston, Miami na Seattle kabla ya kuruka hadi London Uingereza, Turkey Dubai, Indonesia, Kenya, Afrika Kusini na kumalizia Albania,” Rayvanny alijitapa kwa mbwembwe.

Msanii huyo anazidi kutaradadi kwenye safu za mapenzi na muziki haswa baada ya kurudiana na mzazi mwenzake Fahyma.

Wiki jana, charts Tanzania ilitoa takwimu zilizoonesha Rayvanny kwa mara ya kwanza kumdungua Diamond kwenye wasanii waliotazamwa Zaidi katika YouTube kwa mwezi Aprili.

Chanzo: Radio Jambo