Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny afikisha views bilioni 1

Rayvanny Mksd Rayvanny afikisha views bilioni 1

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni CEO wa Lebo ya Next Level Music, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ameweka rekodi yak wake mwenyewe kwa kufanikiwa kufikisha watazamaji (views) bilioni moja kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni miaka saba tangu ajiunge na mtandao huo huku akigonga wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 4.66.

Rayvanny anakuwa msanii wa pili nchini Tanzania kufikisha watazamaji zaidi ya bilioni moja akiwa nyuma ya bosi wake wa zamani, Diamond Platnumz ambaye kwa sasa ana watazamaji zaidi ya bilioni mbili kwenye mtandao huo.

Vanny Boy alifungua channel yake ya YouTube, Machi 17, 2016 na siku iliyofuata akapandisha video yake ya kwanza kwenye mtandao huo ambapo ilikuwa ni interview ya kwanza aliyofanya kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio akitambulisha ngoma yake ya kwanza ya ‘Kwetu’ akiwa msanii wa pili kusainiwa na WCB baada ya Harmonize.

Rayvanny amekuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati kufanya shoo kwenye tuzo za MTVEmma akiwa na Maluma. Pia, ameshinda tuzo ya Diafa mwaka jana 2022 na tuzo ya BET.

Vanny ndiye msanii anayetajwa kuingiza pesa nyingi zaidi kupitia digital platforms zinazouza musiki mtandaoni kama YouTube, Boomplay, iTunes na mitandao mingine.

Tanzania kuna YouTube channe 6 pekee ambazo zimeshafikisha zaidi ya watazamaji bilioni 1 tangu zianzishwe.

1. Diamond POlatnumz – bilioni 2.323

2. Millard Ayo – bilioni 1.781

3. Global TV Online – bilioni 1.487

4. Yess Jamal – bilioni 1.303

5. Wasafi Media – bilioni 1.053

6. Rayavanny – bilioni 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live