Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny adaiwa kuingia mitini licha ya kulipwa pesa ya kolabo

Queen Marie J Rayvanny Rayvanny adaiwa kuingia mitini licha ya kulipwa pesa ya kolabo

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Marie Njoroge, kutoka Kenya almaarufu Queen Marie J amedai kolabo (ushirikiano) yake na msanii wa Bongo Fleva Rayvanny umekwama baada ya Mtanzania huyo kukiuka masharti ya makubaliano yao.

Rayvanny ameingia katika shutuma hizo baada ya Marie J kudai kuwa aliwasiliana na msanii huyo maarufu Bongo kupitia WhatsApp, na kwamba alikubali kumsaidia kumuinua katika tasnia hiyo kwa kufanya naye kazi.

“Rayvanny alikiuka masharti ya makubaliano tuliyokuwa nayo ya kufanya kazi kwa ushirikiano hata baada ya gharama zote za uzalishaji kufanywa," aliambia gazeti la Pulse kwenye mahojiano.

"Aliomba nimpe kiasi cha pesa anisaidie ndani ya muda mfupi hivyo tulikubali na nilikuwa nikimtumia pesa wakati wowote anaoomba."

Aliongeza kuwa ushirikiano na msanii huyo wa zamani wa Wasafi Records ulipaswa kutolewa mnamo 2020.

Hata hivyo, alidai, Rayvanny baadaye alim-block kwenye mitandao yote ya kijamii yote, akisingizia kwamba "kuna mambo yametokea" bila ufafanuzi mwingine wowote, na kuacha mpango huo bila mwelekeo.

Queen Marie J hata hivyo bado ana matumaini kuwa kolabo hiyo na Rayvanny itazaa matunda, akisema labda ilikwamishwa na rekodi yake ya zamani lakini kwa vile aliondoka na sasa yuko peke yake, wanaweza kuifufua tena.

“Alitakiwa kunisaidia mimi binafsi lakini kwa kuwa ameachana na lebo yake ya awali itakuwa rahisi kufanya naye kazi, hivyo natumai mambo mazuri zaidi. Labda shida ilikuwa lebo yake wakati huo, "alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live