Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny, Paula, Fahyma Watajwa Kwenye Tuzo

Paula Fahyma Rayvanny, Paula, Fahyma Watajwa Kwenye Tuzo

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMITINDO na mzazi mwenza wa Staa wa Bongofleva, Raymond Mwakyusa ' Rayvanny', Faima Msenga 'Fahyma au Fahyvanny' na mpenzi wa sasa wa Rayvanny, Paula Paul Matthysse 'Paulah Kajala kwa pomoja wametajwa kupata tuzo za 'AfroSwagga Awards 2021' zinazohusu masuala ya mtindo na urembo.

Mastaa hao wametajwa katika vipengele tofauti huku wakishindanishwa na mastaa wengine wa Bongo ambao pia wapo kwenye tasnia hiyo ya urembo na mitindo

Katia tuzo hizo, Rayvanny na mpenzi wake Paulah kwa pamoja wamesinda tuzo hiyo katika kipengele cha 'Best Fashionable Couple Of the Year', huku Fahyma yeye akishinda katika kipengele cha "Best Red Carpet Event Sensation".

Mbali na hivyo pia Paula ameshinda pia tuzo hiyo katika kipengele cha 'Best Upcoming Fashion Influencer' huku watu wengine maarufu kama Gigy-Money, Chris Mziwanda, Mange kimambi na #Hamisa Mobetto wakishinda tuzo hiyo pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live