Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny: Mimi ni msanii huru

Rayvanny Mm Rayvanny

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa lebo ya NLM, raymond Mwakyusa 'Rayvanny' ameamua kufunguka kuwa yeye ni msanii huru na hayupo chini ya mtu yeyote badala yake yuko na management yake mpya.

Kauli hiyo ya Rayvanny inakuja ikiwa ni siku moja baada ya kuenea kwa taarifa kuwa anatakiwa kulipa pesa kiasi cha Tsh milioni 50 kwa lebo yake ya zamani ya WCB kufuatia msanii huyo kupanda jukwaani na kutumbuiza wakati wa Nandy Festival iliyofanyika hivi karibuni mjini Songea ilihali hajamlizana kikamilifu na WCB.

Ikumbukwe kuwa, Rrayvanny aliondoka hivi karibuni WCB baada ya kufanya nayo kazi kwa miaka sita. Lakini baadaye taarifa zikasambaa kuwa tayari ameshamalizana na WCB baada ya kulipa kiasi cha Tsh milioni 800 alizotakiwa kulipa ili kuondpoka katika lebo hiyo.

Siku chache baadaye, Rayvanny na mabosi wake wa zamani, Diamond Platnumz na Sallam SK wote watatu kwa pamoja walionekana katika viunga vya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) huku kukitajwa kuwepo na kikao kizito cha makubaliano baina yao ili Rayvanny aweze kumalizana kikamilifu na WCB.

Kitendo cha kuonekana BASATA kilidhihirisha kuwa msanii huyo na lebo yake bado hawajamalizana kikamilifu licha ya pande zote mbili kutokuwa tamko lolote mpaka sasa iwapo wamemalizana au lah!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live