Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny, Marioo: Ni muda wetu

Rayvanny Marioo Rayvanny, Marioo: Ni muda wetu

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni muda wetu! Ndivyo wanavyotamba wakali wawili kunako Bongo Flevani, Rayvanny na Marioo baada ya kuonekana wakiwa studio katika shughuli rasmi ya kuandaa ngoma mpya.

Ifahamike kwamba ngoma ya mwisho ambacho Rayvanny au Chui alimshirikisha Marioo ilikuwa ni Te Quiero ambayo ilifanya vizuri katika chati za muziki ndani ya Bongo na Afrika Mashariki.

Kwa mujibu ya wawili hao, maprodyuza wa ngoma hiyo ni S2kizzy na Soundboy.

Ngoma hiyo inatarajiwa kuruka hewani wakati ambapo Marioo anazidi kufanya vizuri kimuziki kwa nyimbo zake ambazo zimetokea kupendwa na mashabiki wengi.

Kwa upande wake, Rayvanny amehusishwa na kuondoka WCB ila anashikilia kwamba wakati ukifika ataondoka bila vurugu yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live