Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny, Lil Romeo kukutana uso kwa uso

Lil Romeo Na Rayvanny.png Rayvanny, Lil Romeo kukutana uso kwa uso

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa kizazi kipya Raymond Mwakyusa, maarufu kama 'Rayvanny' anatarajia kukutana uso kwa uso na msanii wa Marekani Lil Romeo katika tamasha la Masai Global festival litakalofanyika Arusha Agosti 9-10.

Tamasha hilo litakalofanyika siku mbili lina lengo la kutangaza vitutio vilivyoko nchini sambamba na kuunganisha maswala ya Utamaduni na Sanaa katika kuvutia watalii nchini.

Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi wa Masai Global festival, Saidy Lukembo amesema kuwa zaidi ya wageni na watalii 5000 wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kujifunza na kufurahia tamaduni za kitanzania, ambapo wasanii hao watatoa burudani kwa kushirikiana na wengine wa Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live