Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny: Hakuna sababu ya kugombana na Diamond, Harmonize

Diamond Harmonize Rayvanny Muziki.jpeg Rayvanny: Hakuna sababu ya kugombana na Diamond, Harmonize

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Rayvanny, amefunguka kuhusu namna ambavyo maisha yake kwa sasa yalivyo na kusema kuwa yeye ni mtu wa kupenda amani, Licha ya kutoka kwenye lebo yake ya zamani WCB amesisitiza kuwa bado wanamahusiano mazuri na wameweza kuitunza amani, na maisha yanaendelea.

Rayvanny amezungumza hayo hii ni baada ya kuwasili nchini Tanzania akitokea nchini Kenya ambapo kulifanyika ugawaji wa Tuzo za EAEA (East Africa Entertainment Awards) usiku wa kuamkia Jumatatu na kunyakuwa Tuzo tano katika vipengele tofauti tofauti.

"Ndiyo maana niliposti kwenye birthday ya Harmonize, ninapenda sana kuishi kwa Amani badala ya vita.

"Kama ambavyo nimetoka Wasafi, changamoto zilikuwa nyingi lakini tumeweza kuitunza Amani na maisha mengine yanaendelea. Mtu mwingine anajua zikishatoka pesa unanua, vita kwamba ninatoaje mahela yote hayo? Lakini mwisho wa siku tunafanya kazi na biashara, familia lazima iendelee kuwepo.

"Kitu hicho nilikuwa nikimwambia Harmonize na hata Diamond alikiona, nilikuwa na kila sababu ya kusema tunagombana lakini tuliitunza amani, nikamwambia hakuna sababu ya kuendelea kugombana. Hata Harmonize ameshasema mara kibao kwamba ni wakati wa kuwa na amani na Diamond.

"Mwingine anaweza kusema tunapunguza utamu wa game, nadhani hauwezi kupungua kama mnaongea kila mmoja atatoa kazi kali na ushindani utaanzia ndani na kupata mafanikio. Ni vizuri kuwa na amani na kumaliza tofauti zetu kwa sababu vita inaishiaga sehemu mbaya na inaumiza vizazi," amesema Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live