Inawezekana penzi la kurudiana likawa lina raha yake! Staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa 'Rayvanny' na Fahyma ni kama vile gari limewaka upya.
Sasa hivi wanaoneshana mahaba kama yote na kuposti kwenye ukurasa wa Instagram na tukio jipya ni mwamba kwenda kumpokea mpenzi wake huyoa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mpenzi wake huyo alikuwa akitokea Uturuki kwenye shughuli zake za biashara na alipotua, jamaa alienda kumpokea akiwa na mabaunsa wake ambao walimshikia mwavuli.
Wakiwa wanatembea kuelekea kwenye eneo aliloegesha gari, walikuwa wakibusiana mara kwa mara kuonesha walikuwa wamemisiana.
Wawili hao ambao wana mtoto mmoja, walikuwa wapenzi zamani wakaachana na kisha hivi karibuni wamerudiana na penzi lao limekuwa lamoto balaa.