Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ray afunguka siri nzito kuhusu Kanumba

Ray Kanumbaaa Ms.jpeg Ray afunguka siri nzito kuhusu Kanumba

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe kutokea kwenye kiwanda cha Bongo Movie, Vincent Kigosi 'Ray' jana Novemba 25, 2022 amezungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza dili lake jipya na kampuni ya ulinzi nchini #K4SSecurity kama balozi mpya wa kampuni hiyo.

Mbali na Jambo hilo ambalo ndilo lililokuwa lengo hasa la press conference yake, Ray amedokeza ujio wa kazi zake mpya na kubwa, lakini pia ametaja sababu kubwa ya kudumaa kwa tasnia ya uigizaji nchini, ni kutokuzalishwa kwa waigizaji wapya wenye vipaji vya kufikia levo za kina Wema Sepetu.

Ray amedai anarudi kwenye sanaa kuiboresha upya kwa kuleta vipaji vipya kwa sababu ana karama hiyo ya kuibua talents kali.

Aidha, mkongwe huyo wa filamu za Bongo amedai anashangaa watu wakisema alikuwa anabebwa na Kanumba, wakati Kanumba alitokea kwenye mikono ya Ray, waigizaji kama Uwoya, Wolper, Johari na wengine kibao wakubwa kama Thea walitokea kwenye mikono yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live