Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba ya usaili Miss Tanzania 2020 hii hapa

Ratiba ya usaili Miss Tanzania 2020 hii hapa

Sat, 7 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Je,  wewe ni binti wa Kitanzania mrembo na unadhani una sifa zote za kuwa mrembo wa Taifa yaani Miss Tanzania 2020?

Kama ndiyo,  Kamati ya Miss Tanzania itaanza kufanya usahili wa kanda zote nchini  sambamba na kutafuta vipaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Miss TanzaniaBasila Mwanukuzi imeeleza wasichana wanaoamini wana sifa wajaze fomu ya maombi inayopatikana kwenye tovuti ya Miss Tanzania www.misstanzania.co.tz na mwisho wa kurudisha fomu ni Januari  31, 2020. 

Amesema wataanza kufanya usaili Machi , 2020 watakuwa Kanda ya Kati (Dodoma), Kanda ya Vyuo Vikuu (Dar) na  Kanda ya Ziwa (Shinyanga).

Amsema Aprili, 2020  utafanyika  Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) na Kanda ya Mashariki (Morogoro).

Ameleza usaili Kanda ya Dar es Salaam utafanyika Mei,  2020.

“Hii ni  fursa ya pekee ya kupata nafasi ya kuwakilisha nchi katika fainali za mashindano makubwa duniani ya urembo ya Miss world 2020.”

“Pia utapata nafasi ya kuonyesha kipaji chako sambamba na mradi wako wa kazi za jamii ‘beauty with a purpose’ na kutangaza nchi yako kitaifa na kimataifa katika kutangaza utalii tamaduni sanaa na urembo,” amesema Mwanukuzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz