Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi familia ya Diamond yamkubali Zuchu

Familia Ya Mondi Rasmi familia ya Diamond yamkubali Zuchu

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa hali ilivyo sasa, ni dhahiri sasa, msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othman 'Zuchu' ameshakubalika ukweni kwake na sasa familia nzima ya Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' imempitisha mrembo huyo kama mkwe wao.

Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa, awali mama Diamond alikuwa mzito kumkubali Zuchu kutokana na kuwa na mahaba sana na mzazi mwenziye Diamond, Zari lakini kwa sasa ameshakubali yaishe na nguvu zake amezielekeza kwa Zuchu.

Tanzaniaweb imefatilia post za hivi karibuni za mama Diamond na kuona akiandika jumbe ambazo zinaashiria wazi kwamba, amebariki Zuchu kuwa mkwewe.

"MUIMBA TARAAB MASHUHURI WA WCB ZUHURA OTHMAN SUOD @officialzuchu ALAFU MKWE WANGU MIMI HAPA ATIMAE LEO KAIPELEKA MIONDOKO HIYO NCHINI MAREKANI JE ATATOBOA,,,??? NAKUTAKIA SHOW NJEMA MAMA," aliandika kwa herufu kubwa mama Diamond.

Kwa upande wake kaka wa Diamond, Romy Jones naye amedhihirisha hilo alipompongeza Zuchu baada ya kushinda tuzo hivi karibuni.

"This is soo touching,emotional...My sister,friend, shemeji lol."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live