Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Rayvanny na Fahyma wamerudiana

Rayvanny Fahyma Mtoto Rasmi: Rayvanny na Fahyma wamerudiana

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Awali kulikuwa na tetesi nyingi kuwa, msanii Rayvanny amerudiana na mpenzi wake, mrembo Paula Kajala, lakini kumbe mambo yalikuwa ni tofauti kwani aliyerudiwa ni Fahyma; baby mama wa jamaa huyo.

Hii ni baada ya Rayvanny kumposti Fahyma kwenye Snapchat, jambo ambalo hajalifanya yapata miaka miwili sasa.

Kitendo hicho kimemuibua Paula ambaye kwa sasa anarusha vijembe kwa Rayvanny huku akimsifia Harmonize ambaye ni mchumba wa mama yake, Kajala Masanja.

Katika moja ya posti zake, Paula anaimba wimbo wa Harmonize wa Bakheresa akiwaponda wanaume ambao ni bahili huku akimsifia Harmonize kwa kuweza kumuhonga mama yake magari mawili ya kifahari aina ya Range Rover zenye majina ya Kajala 1 na Kajala 2.

Wengi wanaamini hilo ni dongo kwa Rayvanny ambaye inasemekana ni bahili wa kutupwa kwani alishindwa kumfanyia Paula makubwa ikiwemo kumfungulia duka la nguo, jambo ambalo Harmonize amelifanikisha.

Sasa; kama kawaida yake, Fahyma ameanza kutamba kwamba yeye ni mwanamke mzuri sana na haiwezekani mwanaume akamuacha na akifanya hivyo, atarudi tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live