Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Harnmonize kuzichapa 'live' na Mwakinyo

Harmonize Mwakinyo Zzz Harmonize na Mwakinyo.

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kuwa wapo kwenye mkakati wa kukamilisha vitu vyote muhimu na kuweka mambo sawa yeye na bondia namba moja nchini, Hassan Mwakinyo ili waweze kupanda ulingoni kuzichapa.

Harmonize amesema kuwa pambano hilo litakuwa si la ubingwa bali ni pambano la hisani ambapo pesa itakayopatikana kutokana na pambano hilo itatolewa kwa ajili ya kuwasaidia wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa wa kansa na watoto yatimaa.

“Mwakinyo kupigwa atapigwa na atapigwa kwa faida ya watu wengine. Lakini kwa sasa tunge-focus tunasheherekea vipi Album yangu mpya ya MUZIKI WA MAMA SAMIA, haya yeye nimemwalika atakuwepo kwenye event.

“Watu wanashindwa kuelewa kuwa pambano letu sisi sio la ugomvi, am the best he is the best, sasa kwa nini tusitumie hii nafasi tukaingia ulingoni, no feelings, lakini pia kitakachopatikana kitaenda kusaidia wenye uhitaji. Kuna watu wanapambania kansa, HIV, kuna mayatima mtaani na hao ndio mashabiki wenyewe.

“Ndiyo mashabiki wa harmonize na ndiyo mashabiki wa Mwakinyo, wanapenda muziki wetu, wanapenda boxing. Lakini pia kwenye burudani kusiwe na kitu kilekile, kunatakiwa kuwe na kitu kipya. Kwa hiyo pambano letu there is no hard feelings kabisa,” amesema Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live