Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Diamond ajilipua kwa Zuchu

Diamond Zuchu 1551252017 Diamond na Zuchu

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amemwonyesha mapenzi msanii wake Zuchu baada ya kununua gari jipya aina ya Range Rover.

Zuchu ambaye anadaiwa kutengana na Diamond majuzi baada ya kutoka naye kwa muda alinunua Range Rover nyeusi na kupakia picha kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia kwa mtandao wa Instagram, Diamond alimshangilia Zuchu akisema kuwa amemfanya kujivunia kiasi cha kutemebea kifua mbele.

"Unajua kunifanya nitembee kifua mbele Zuuh. Naomba kuanzia leo nirasimishe rasmi kuwa Range ni gari maalum kwa ajili ya Queens wote," Diamond alisema.

Februari mwaka huu Zuchu alitangaza roho yake kulia machozi baada ya penzi kugeuka mwiba - yaani kutemwa na mpenzi wake aliyeaminika kuwa Diamond.

Kupitia mtandao wa Snapchat, kipusa huyo alisema kwa sasa yuko singo na kuwataka mashabiki wake kutomgusia lolote kuhusiana na mpenziwe.

Aidha, inaarifiwa Zuchu alihakikisha kuwa amefuta picha zake zote na msanii wa Bongo Diamond Platinumz.

Wawili hao walikuwa wakidaiwa kuwa wapenzi tangu mwaka wa 2022 Diamond alipoonekana kumsongea Zuchu.

"Msinitie kamba kwenye mambo yake, kwa sasa mimi niko singo," alisema kwenye ujumbe wake kwa mashabiki.

Ujumbe wake ulijiri siku tatu tu baada ya wawili hao kufurahia siku ya Valentino kwa jumbe za mapenzi kali jambo ambalo linafanya wengi kushuku kinachoendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: