Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Davido atangaza ndoa na Chioma

 108765264 Davido1 Rasmi: Davido atangaza ndoa na Chioma

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Davido yupo mbioni kuaga kambi ya ukapera, amethibitisha rasmi atafunga ndoa na bibie Chioma maarufu Chef Chi ambaye anatajwa kuwa ni mjamzito kwa sasa.

Davido amebainisha hayo akiwa na baby mama wake huyo pamoja na mchungaji wake Tobi Adegboyega huko Uingereza, alipoenda kumtambulisha Chioma kwa mchungaji huyo.

“Our wife, our real wife,” anasikika Mchungaji Tobi akieleza, na Davido akaongezea, “Hundred per cent, going down 2023.”

Ikumbukwe, Davido na Chioma walianza mahusiano yao tangu mwaka 2017, na 2019 Davido alimvisha pete ya uchumba Chioma.

Hata hivyo wakaja kuachana mwaka 2020, wakabaki kuwa walezi wa mtoto wao. Julai mwaka huu wakawa wanahusishwa kurudiana, kisha baadae wakathibitisha na sasa wamepanga kufunga pingu za maisha ifikapo mwakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live