Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi! Ben Pol na Anerlisa wameachana, talaka yakamilika

Anerlisa BENPOL Ben Pol na Anerlisa

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sasa ni rasmi kuwa mfanyabiashara wa Kenya Anerlisa Muigai na mwanamuziki kutoka Tanzania Ben Pol sio mke na mume tena.

Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja kupitia ukurasa wake wa Instagram, amefichua kuwa talaka yake na mwimbaji huyo wa Bongofleva hatimaye imekamilika.

Mrembo huyo amewashukuru mawakili wake kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa talaka yake umekamilika

“Niko huru rasmi. Haitakuwa sawa kutowatambua mawakili hawa wawili ambao walifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba talaka inafanywa haraka na sio kusubiri kwa miaka. Hamza Jabir na Hosea Chamba, asanteni kwa kazi zenu na kwa kufanya kila kitu mlivyoombwa.” alisema kwenye Insta stori.

Anerlisa na Ben Pol walifunga ndoa Mei mwaka 2020 lakini wakatengana mwaka jana ambapo Ben Pol aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live