Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rapcha akana kubanwa koo na Majani

Rapcha 2 Rapcha akana kubanwa koo na Majani

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Last King Of 90’s, Rapcha amekanusha taarifa za kupangiwa kitu cha kuzungumza awapo kwenye interviews na bosi wake P-Funk Majani baada uvumi kuenea kuwa kuna baadhi ya vitu hatolei ufafanuzi kutokana na kubanwa koo.

Akipiga stori na East Africa Tv, msanii huyo wa Bongo Records amesema haijawahi tokea akazuiliwa au kupangiwa vitu vya kuzunguma kwani ana amini yeye sio miyeyusho.

"Haiwezi kutokea kitu kama hicho, ujuwe mpaka mtu anakupangia cha kuzungumza basi anajua kuwa huwa unafyatuka ila kwa mtu ambaye ana amini katika msanii wake na anajuwa kuwa hana miyeyusho hawezi kumpangia cha kuzungumza" - Rapcha

Chanzo: eatv.tv