Rapa wa Ufaransa Mohamed Sylla almaarufu kama MHD amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa mauaji ya kijana mmoja yaliyokea jijini Paris mwaka 2018.
MHD alikutwa na hatia ya kumuua Loic K (23). Katika kesi hiyo washtakiwa wengine watano nao wamehukumiwa vifungu vya kati ya miaka 10 na 18, huku wanaume watatu wakiachiwa huru.
Katika tamko lake la mwisho Mahakamani, MHD alisisitiza kuwa hana hatia.
Loic K alifariki dunia Julai 5, 2018 baada ya kuzingwa na gari jeusi aina ya Mercedez, baadae kupigwa vibaya na kuchomwa visu na kundi la watu.
Rapa huyo alikana kuwepo kwenye eneo la tukio, hata hivyo mkazi mmoja wa eneo hilo alirekodi shambulio kutokea dirishani mwake na iligundulika kuwa gari ile ilikuwa ikimilikiwa na msanii MHD.
Baadhi ya mashahidi walimtambua MHD kwenye video hiyo kwa kutumia sweta lake pamoja na staili ya nywele.