Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rapa Snoop Dogg kurekodi muziki wa Gospel

800 Snoop Dogg Is Delving Into Gospel Music 660x400 TZW

Sat, 30 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Mtu wangu wa nguvu huu ndio wakati wa kufanya maazimio ya mwaka Mpya 2018 na watu wengi huwa makini kabisa kuweza kufanya mikakati ya kutosha, sasa moja ya watu waliofanya maazimio ni Rapa Snoop Dogg ambaye amekuwa kwenye muziki Hip hop na RnB kwa takriban miaka 20. Sasa anataka kufanya kitu kipya mwaka 2018.

Akizungumza na Billboard Snop amesema: “Nimekuwa nikitaka kujaribu kufanya muziki wa injili. Hii inaweza kushangaza watu wengi lakini mbali na yote mimi napenda kusema niko tayari kwa ajili ya maisha mapya ya muziki katika mwaka mpya wa 2018!”

Tunapaswa kumbuka kwamba SNOOP aliamua kuwa rasta na hata akabadilisha jina lake Snoop Lion miaka michache iliyopita. Amefafanua hayo wakati akizungumza kuhusu video yake mpya  aliyoipa jina  ‘My Last Name’, ambayo ilikuwa Dedication kwa mke wake Shante Broadus.

Je! Upo tayari kwa ajili ya muziki wa  injili toka kwa Snoop?

MAGARI YALIYOUZWA SANA 2017 SHOW ROOM ZA ARUSHA, BONYEZA PLAY KUTAZAMA

BAADA YA WATOTO WA ZARI KUTOONEKANA KWENYE BIRTHDAY PARTY YA MDOGO WAO (NILLAN), BONYEZA PLAY KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com