Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rapa Mr Teacher alia na maisha ya Watanzania kupitia wimbo ‘Thomas Sankara’ (Audio)

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Thomas Sankara sio jina geni kwa Waafrika wengi kutokana na umaarufu wa muasisi wa Taifa la Burkina Faso.



Mr Teacher

Rapa mtanzania ambaye anaishi nchini Marekani, Julius Haule aka Mr Teacher ameachia wimbo wake mpya ambao unakwenda kwa jina la Thomas Sankara, jina la mwanaharakati ambaye alichukua hatua ikiwemo ya kufuta matumizi ya magari ya kifahari,kujikita katika kilimo,afya, michezo na haki za wanawake na mambo mengine mengi na kwa kipindi kifupi nchi hiyo ilitoka katika kuagiza vyakula na kuwa wauzaji wa vyakula nje.

Msanii huyo amesema aliandika wimbo huo kwa lengo la kuwakumbusha watanzania kwamba kila kitu kinawezekana kama mtu ukiamua kupambana kwaajili ya Watanzania.



Mwaka 1999 Mr Teacher aliachia wimbo ‘Stop Killing’ huku akiwa amemshirikisha Nigga J (enzi hizo). Hii ililaani vita na mauwaji na ilidhaminiwa ma amnesty International.

Kwa sasa rapa huyo afanya maandalizi ya video ya ngoma yake mpya ambayo iko kwenye editing stage ya mwisho.

Pia alisema anaendelea kurekodi ngoma nyingine zaidi ambazo ataziachia pamoja na video.

“Lengo langu ni kuelekeza nguvu nyingi katika muziki wangu ili fans wangu waendelee kupata muziki wangu. Ninahitaji support ya fans ili niendelee kuwaletea kazi zenye ubora na ujumbe maridhawa kwasababu mimi binafsi najua kazi ya msanii ni kuelimisha na burudisha,” alisema Mr Teacher.

Nyimbo yake nyingine iliyopita inaitwa, Mheshimiwa Rais.

Chanzo: bongo5.com