Rapa Lil Durk amekamatwa kwa mashtaka ya mauaji ya kulipia (Murder-for-hire) huko Broward, Florida.
Imeripotiwa kuwa mkali huyo wa “All My Life” anashikiliwa bila dhamana, Kukamatwa kwake kunakuja baada washikaji wake watano wa kundi la OTF kukamatwa wakihusishwa na mauaji ya Saviay’a Robinson, binamu wa Rapa Quando Rondo, yaliyotokea mwaka 2022 huko Los Angeles.
Mashtaka yanaonyesha kuwa watu hao wana uhusiano na kundi la Durk, OTF, na wanahusishwa na njama za mauaji zilizopewa msaada wa kifedha na lebo hiyo ya Lil Durk. Mauaji ya Robinson yanadhaniwa kuwa ni kulipiza kisasi kwa kifo cha rafiki wa Lil Durk, na Rapa King Von.