Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Range Rover la Mobeto laibua gumzo

Mobeto Safi Range Rover la Mobeto laibua gumzo

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisa Mobeto; ni mwanamama staa wa muziki, filamu na mitindo nchini Tanzania ambaye wikiendi iliyopita amezua balaa baada kueleza furaha aliyoipta ya kupitiliza baada ya kudai kuzawadiwa gari la kifahari aina ya Range Rover Evogue.

Hamisa aliposti video fupi ikimuonesha akiwa mwenye furaha baada ya kuzawadiwa gari na mpenzi wake ambaye alimficha sura na kusema; “Kuna wanaume, halafu kuna mwanaume wangu mimi hapa, najisikia kulia…”

Hata hivyo, hazikupita saa nyingi sana, kabla ya wafukunyuku kuibuka na video zikionesha Hamisa akipanga ‘script’ ya kujizawadia mwenyewe gari hilo.

Video inamuonesha Hamisa akiwapanga watu wake jinsi watakavyotengeneza tukio ili ionekane anapendwa na mpenzi wake kumbe amejinunulia mwenyewe.

Pamoja na hilo, lakini wenye mawazo chanya kwa Hamisa wanampongeza maana ni gari lake, ila kwa nini aigize kama amezawadiwa?

Wapo wanaosema alichokifanya Hamisa ni ujinga ulioshamiri kwa baadhi ya mastaa Bongo ambapo wanapenda kuishi maisha ya kuigiza.

Wengine wanasema kuwa, bado Hamisa ana hang’over ya penzi la Diamond kwani amefanya hivyo kutokana na kitendo cha mwanawe kutokupostiwa na familia ya jamaa huyo siku ile ya birthday yake.

Wanasema kuwa anachokifanya Hamisa ni kuigiza ana furaha na anajaribu kutengeneza mazingira ionekane na yeye kuna mtu anampenda kiasi cha kumzawadia gari la kifahari aina ya Range Rover.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live