Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ramesh Babu; Kinyozi bilionea anayemiliki magari 400

Ramesh Babu.jpeg Ramesh Babu; Kinyozi bilionea anayemiliki magari 400

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: Habari leo

Ramesh Babu, ni ‘Bilionea Kinyozi’ aliyekulia katika familia iliyokuwa ikishindia mlo mmoja kwa siku. Baada ya kifo cha babake, mama yake hakuweza kuendelea na saluni iliyokuwa ikimilikiwa na familia na aliamua kuikodisha ili alipwe Rupia 5 (Sh 140) kwa siku.

Ramesh Babu alifanya kila kazi katika maisha yake yote ya utotoni kumsaidia mama yake kutengeneza senti chache za ziada. Ramesh Babu alianza kazi ya muda ya usambazaji magazeti, maziwa na kila kitu ambacho kiliwezekana akiwa na umri wa miaka 13 kusaidia familia yake.

Baada ya kumaliza darasa la kumi, Ramesh Babu aliamua kuendelea na saluni ya baba yake. Saluni hiyo ilipewa jina la ‘Inner Space’ na ilikuwa katika eneo la maduka karibu na shule aliyosomea.

Babu alikusanya pesa kutoka saluni yake na kununua gari la Maruti Van (Omni) kutoka kwa akiba ya pesa zake mwenyewe na msaada wa mjomba wake mwaka 1993. Alikuwa akiikodisha muda mwingi alipo kuwa na wateja wengi saluni bila kujua kazi hiyo ingemfanya kuwa bilionea!

Ramesh alipewa kandarasi yake ya kwanza ya biashara na Intel kwa usaidizi wa mama yake aliyekuwa akifanya kazi za usafi. Polepole akakusanya msingi mzuri wa wateja, Ramesh alitambua uwezekano wa kuanzisha huduma ya juu ya kukodisha magari na kuanza kujenga kundi la magari.

Leo Ramesh ndiye mmiliki wa Ramesh Tours and Travels na amekuwa akinunua magari ya bei ghali kwa takriban miaka 30 sasa. Amekuwa akikodisha magari ya kifahari kwa mwaka mzima sasa, kuanzia mwishoni mwa miaka ya 90.

Ramesh ni miongoni mwa mabilionea kadhaa wanaopenda magari. Wengine wanao miliki magari zaidi ya 400 ni pamoja na Paul Riddic kutoka Uingereza aliyekuwa akipenda magari ya kwenda haraka na Rodger Dudding ambaye pia ni mwingereza.

Kwenye ripoti za CAG wiki hii tumeona baadhi ya taasisi za umma zimelipia magari 21 kwa zaidi ya bilioni 4 na bado hayajakabidhiwa kwa kipindi cha karibu miezi 28.

Katika orodha hiyo, Wizara moja imeagiza magari mawili (2) kwa gharama ya Sh bilioni 1.6

Chanzo: Habari leo