Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rama Dee adai kupigwa vizinga na wasanii wa Bongo

Rama Dee Rama Dee adai kupigwa vizinga na wasanii wa Bongo

Mon, 4 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe na mkali wa RnB Rama Dee, amesema kutokana na tatizo la Corona nchini Australia, limemfanya kukaa ndani kwa miezi miwili na kutokwenda kazini kwa muda wa miezi 6.

Rama Dee amesema licha ya kukaa ndani kwa muda wote huo, analipwa kama kawaida na kuna baadhi ya kazi za kiofisi anazifanya akiwa nyumbani, lakini anashangaa kuona kuna baadhi ya wasanii wanaachia kazi nzuri lakini bado wanamuomba pesa.

Akieleza hayo kupitia show ya Dadaz ya East Africa Tv, Rama Dee amesema muziki wa Bongo ni local sana na yeye binafsi ameacha kuimba miaka miwili iliyopita.

"Mziki wa Tanzania upo local sana, sasa hivi nimefanya mapumziko ya kufanya muziki kwa miaka miwili, kati ya hii miaka miwili niliyopumzika nimeona wasanii wengi kazi zao zimefanya vizuri lakini nikikuonyesha meseji utaona wanavyonipiga vizinga" amesema Rama Dee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live