Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia amsaidia matibabu Haitham

MwanaFA Na HARMONIZE Rais Samia amsaidia matibabu Haitham

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Harmonize kupaza sauti yake kwenye shoo yake visiwani Zanzibar, hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amemwezesha msanii Haitham kupatiwa matibabu.

Kupitia Insta Story yake, Harmonize aliposti kipande cha maelezo yake akimshukuru Naibu Waziri wa Sanaa na Utamaduni Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' kwa kupokea maelekezo ya Rais Samia na kuyafanyia kazi kwa haraka.

“Yeeees! Wakati Dr. Samia Suluhu Hassan anamteua Mh Naibu Waziri Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ katika wizara hii ya Tamaduni, Sanaa na Michezo, wapenda maendeleo tulijipiga kifuani maana tulijua licha ya kuujua muziki wa Tanzania na tamaduni zetu, anatujua kwa majina mmoja baada ya mwingine.

“Hongera sana bro, simu moja everything sorted matibabu yanaendelea tena ya uhakika zaidi mambo ya kupaza sauti tuyasahau katika kipindi hilki cha uongozi wa mama Samia hadi raha!! Get well soon haitham we love you, ameen.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live